Mtandaomall
@mtandaomall
JAMBO LA PILI: WAELIMISHE WATEJA JINSI BIDHAA AU HUDUMA YAKO INAVYOWASAIDIA. Kama unafanya biashara mtandaoni au unapanga kuanza, usijikite kwenye kutangaza bidhaa au huduma yako pekee. Jifunze kuwaeleza watu kwa nini wanahitaji kile unachokitoa. โ Waoneshe changamoto wanazokutana nazo katika maisha au biashara zao. โ Waeleze jinsi bidhaa au huduma yako inavyoweza kuwasaidia kutatua changamoto hizo. โ Waambie faida na ubora wa kile unachokitoa, na kwa nini wanapaswa kukichagua. โ Toa mifano halisi inayoonesha namna huduma yako inavyoweza kuboresha maisha au biashara zao. Kumbuka: Wateja hawahitaji kusikia tu kwamba una bidhaa nzuri. Wanahitaji kuelewa bidhaa hiyo itawasaidia nini na kwa nini wanapaswa kukuchagua wewe. Unapojenga akaunti yako ya Instagram, Facebook, TikTok au mtandao mwingine wa kijamii, hakikisha maudhui yako yanaelimisha, yanajenga uaminifu na yanaonesha suluhisho unalotoa. Usiwe mtu wa kutangaza tu. Kuwa mtu wa kutatua matatizo kupitia bidhaa au huduma yako. Anza kujenga biashara yako kwa kutoa thamani kabla ya kuomba mauzo. ๐ Follow Mtandao Plus kwa elimu zaidi kuhusu biashara mtandaoni, digital marketing, social media management na namna ya kutengeneza kipato kupitia mitandao ya kijamii. #BiasharaMtandaoni #DigitalMarketingTanzania #SocialMediaMarketing #JinsiYaKupataWateja #MtandaoPlus
Nov 5, 2026